23 Aprili 2025 - 23:37
Source: Parstoday
Wakuu wa taasisi za elimu ya juu Marekani waungana kupinga sera za elimu za Trump

Zaidi ya marais 100 wa vyuo vikuu na taasisi za elimu wamechapisha taarifa ya pamoja wakipinga sera za utawala wa Rais Donald Trump kwa taasisi za elimu ya juu, baada ya Chuo Kikuu cha Harvard kusema utawala huo unatishia uhuru wake.

Taarifa hiyo, iliyotiwa saini na marais kutoka taasisi kama vile Princeton, Brown, Chuo Kikuu cha Hawaii na Chuo Kikuu cha Connecticut State Community, imekosoa kile ilichoeleza kama "unyanyasaji wa serikali na uingiliaji wa kisiasa ambao sasa unahatarisha elimu ya juu ya Marekani."

"Tuko tayari kufanya mageuzi yenye kujenga na hatupingi usimamizi halali wa serikali," ilisema taarifa hiyo. "Hata hivyo, ni lazima tupinge uingiliaji usiofaa wa serikali katika maisha ya wale wanaojifunza, wanaoishi na kufanya kazi kwenye vyuo vyetu."

Taarifa hiyo ya pamoja ni ya karibuni kabisa ya upinzani kutoka viongozi wa elimu ya juu kwa serikali ya Trump ambayo inatumia shinikizo la kutaka ufadhili wa kifedha ili kurekebisha mifumo ya kielimu.

Aprili 14 Chuo Kikuu cha Harvard kilikataa matakwa mengi ya utawala wa Trump, likiwemo la utawala huo kutaka kusimamia serikali ya wanafunzi ya Harvard, vitivo na mitaala ili kuzuia itikadi za kiliberali.

Maandamano ya wanafunzi wanaounga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala katili wa Kizayuni yaliyoanza katika Chuo Kikuu cha Columbia huko Marekani licha ya kukabiliwa na ukandamizaji na ukatili wa mamlaka ya Marekani yalienea kwa mara ya kwanza katika vyuo vikuu vingine vya nchi hiyo. Kuongezeka maandamano dhidi ya Israel kuumeifanya serikali yay Trump kuvishinikiza vyuo vikuu na taasisi za elimu za nchi hiyo.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha